Jeremiah 49:23-27

23 aKuhusu Dameski: “Hamathi na Arpadi imetahayarika,
kwa kuwa wamesikia habari mbaya.
Wamevunjika moyo na wametaabika
kama bahari iliyochafuka.

24 bDameski amedhoofika,
amegeuka na kukimbia,
hofu ya ghafula imemkamata sana;
amepatwa na uchungu na maumivu,
maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

25 Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa,
mji ambao ninaupenda?

26 cHakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;
askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

27 d“Nitatia moto kuta za Dameski;
utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Ujumbe Kuhusu Kedari Na Hazori

Copyright information for SwhKC